Lipa ukitumia
Google
Inachukua sekunde tu kuweka mipangilio — kulipa kwa urahisi kila wakati
Kufanya malipo kwa urahisi kwenye vifaa vyako vyote huanza kwa hatua chache za haraka. Weka maelezo ya kadi yako kwenye Akaunti yako ya Google na yatahifadhiwa kwa njia salama ili uweze kufanya malipo kwa urahisi zaidi.
Kwa malipo ya mtandaoni yawe makubwa au madogo
Kitufe hiki chenye usaidizi kinakuwezesha kufurahia hali ya kulipa iliyorahisishwa na usalama wa ziada kwa kutumia maelezo yako yaliyohifadhiwa.
Miamala kwa njia salama
Ikiwa na vipengele vilivyojumuishwa vya uthibitishaji, usimbaji fiche wa miamala na ulinzi dhidi ya ulaghai, Google Pay husaidia kuhakikisha usalama wa pesa na taarifa zako binafsi. Pia, una uwezo wa kudhibiti kila kitu.